Baraza la Madiwani Halmashauri ya wilaya ya Tarime limelidhia na kupitasha rasimu ya mpango wa bajeti ya mwaka 2021/22, jumla ya kiasi cha sh bilioni 38.27, ikiwa kipaumbele ni miradi ya maendeleo na huduma za jamii kwani kwa kauli moja kiasi sh milioni 185 kutoka mapato ya ndani zimetengwa kulipa deni la madawa bohari ya Dawa (MSD). Pia kiasi cha zaidi ya sh milioni 535 kwa ajili ya kununua mitambo ya barabara. Hivyo kupelekea bajeti hii upande wa miradi ya maendeleo kuchukua asiimia 60 ya mapato ya ndani.
Akisisitiza jambo, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime Mhe. Simion Kiles Samwel wakati wa kufunga mkutano wa baraza la madiwani amesema, fedha hizi sh milioni 185 kutoka mapato ya ndani katika mpango huu wa bajeti zitengwe kwa ajili ya kulipia deni la bohari ya dawa (MSD) ili kata zetu 26 ziweze kupata dawa za kutosha kwa zahanati,vituo vya afya ili kuondoa changamoto za dawa.
Haki miliki ©2017 GWF zimehifadhiwa