Kitengo cha ugavi kinasimamia manunuzi yote toka idara na vitengo vilivyoko kwenye Halmashauri. kitengo hiki kina jumla ya wataalamu saba ambao wanafanya kazi kwa mujibu wa sheria na taratibu za utumishi wa umma.
MAJUKUMU YA KITENGO CHA MANUNUZI:
- Kusimamia manunuzi yote na uuzaji wa mali chakavu kwa zabuni kwenye taasisi isipokuwa kutolea maamuzi ya kisheria na tuzo za mikataba.
- Kuwezesha kazi za zabuni.
- Kutekeleza maamuzi ya bodi ya zabuni.
- Kuandaa mpango wa manunuzi na uuzaji wa mali chakavu kwa taratibu za zabuni.
- Kupendekeza manunuzi na uuzaji wa mali chakavu kwa taratibu za zabuni.
- Kuangalia na kuandaa maelezo ya mahitaji.
- Kuandaa makabrasha ya zabuni.
- Kuandaa matangazo ya zabuni.
- Kuandaa makabrasha ya zabuni..
- Kutoa makabrasha ya mikataba iliyothibitishwa.
- Kutunza kumbukumbu za manunuzi na michakato ya uuzaji wa mali chakavu.
- Kutunza orodha au rejesta ya mikataba yote.
- Kuandaa taarifa ya mwezi kwa bodi ya zabuni.
- Kuandaa na kuwasilisha kwenye vikao vya menejimenti taarifa ya robo ya utekelezaji wa mpango wa manunuzi.
- Kuunganisha manunuzi na uuzaji wa mali chakavu ya Idara zote za taasisi.
- Kutayarisha taarifa zingine zitakazohitajika.
Haki miliki ©2017 GWF zimehifadhiwa